Login to SARIS
Student Information
Management System

28 Feb 2018

Serikali Yatarajia Kuwa na Watoa Hudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Zaidi ya 30,000

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Wadau wa Afya,

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuwa na watoa huduma wa Afya ngazi ya jamii (CHWz) Zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka 2020 katika vijiji Zaidi ya 15,000 nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu katika Mkutano wa Wadau wa Afya, mashirika yasiyo Yakiserikali, na Serikali katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Tunataka itakapofika mwaka 2020, tuwe na angalau Wahudumu wa Afya zaidi ya 30,000 katika vijiji Zaidi ya 15,000 tulivyonavyo Tanzania, Eneo hili tumeliona ni eneo muhimu kwasababu tutapata matokeo ya haraka, ni bora kutumia Bilioni 40 kwa ajili ya kinga ya magonjwa kwa Watanzania .” Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Mhe. Ummy alisema kuwa lengo la Mkutano huo ni kujadiliana na Wadau wa Maendeleo na Mashirika yasiyo Yakiserikali juu ya kuimarisha huduma ya Afya ya msingi hasa katika kuwakinga wananchi dhidi ya maradhi kupitia mikakati ambayo inakubalika kimataifa ya kuwa na watoa huduma katika ngazi ya jamii.