28 Feb 2018

Serikali Yatarajia Kuwa na Watoa Hudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Zaidi ya 30,000

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Wadau wa Afya,

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuwa na watoa huduma wa Afya ngazi ya jamii (CHWz) Zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka 2020 katika vijiji Zaidi ya 15,000 nchini. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu katika Mkutano wa Wadau wa Afya, mashirika yasiyo Yakiserikali, na Serikali katika…